Jumatano, 17 Agosti 2016

HISTORIA BATILI 029

STORY: *HISTORIA BATILI*
MTUNZI: *Mdharuba, J.K.*
+255718274130
mdharuba@gmail.com
www.mdharubajk.blogspot.com
*EPISODE 029*
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
ILIPOISHIA...
Sayyeed anamuua Sheikh Lesangwa bila hata kuagizwa na Mzee J4.
Upande wa pili nako Walter anampa mimba Sarah, shemeji yake Khatib, lakini anakataa wazo la Sarah la kutaka mimba hiyo itoke.
Nuro, Ahmed na Rukia wako katika kikao kizito kutaka kujadili hatma yao katika kazi wanayofanya, Nuro akionekana kuwa na wazo zuri.
Hamida naye anapigiwa simu na Dokta Idd kuhusu mgonjwa anayehisi anafahamiana nae.
Je, nini kinaendelea...

Fuatiliaa.....
“Dokta, naomba unipeleke nimjue huyo mgonjwa tafaadhali” Hamida alimwambia Dokta Idd huku akionyesha kuwa na wasiwasi mkubwa mara tu baada ya kufika pale hospitali na kuonana na Dokta Idd.
“Nifuate” Dokta Iddi alisema bila kuongeza neno lolote jingine.
Wakaongozana mpaka Wadi namba 4 ya hospitali ile, mlangoni paliandikwa *Ward 4-Men*. Wakaingia ndani Dokta Iddi akiwa mbele Hamida nyuma.
“Lahaulaaaa... Baba Abdul.. Jamaaniiii... Nini kimekupata Baba Abdul?” Hamida alihamaki mara tu baada ya kutupa jicho kushoto mwa wadi ile na kumtambua mgonjwa ambaye haswa Dokta Iddi ndiye alitaka aje amtambue.
“Kwa sasa mwache kwanza apumzike, maadamu umeshamtambua” Iddi alimshika mkono Hamida ambaye alikuwa ameinamia kwenye uso wa Khatib aliyekuwa hajitambui kwa wakati huu.
Wakaondoka pale wadini wakielekea katika ofisi ya Dokta Iddi.
“Majina ya huyu mgonjwa yalifanana kabisa na ya yule mwanao Abdul, nikahisi watakuwa na uhusiano, kumbe ni kweli” Dokta Iddi alianza kumuongelesha Hamida wakati akifungua mlango wa kuingia ofisini kwake.
“Ni kweli, yule ndio babaake Abdul”
“Oooh.. Oky, sawa.. Aliletwa hapa na Mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mzee J4, akasema yeye ni msamaria mwema tu ameamua kumleta hapa hospitali. Na pia amenikabidhi funguo za gari alilomleta nalo akidai ni gari yake huyu mgonjwa” Dokta Iddi alitoa maelezo haya huku akifungua droo ya meza yake na kutoa funguo kisha akazitupia pale juu ya meza.
“Mmmh, mbona maelezo hayajanyooka hayo? Ni Mzee gani huyo Dokta jamani?..” Hamida alihitaji ufafanuzi zaidi juu ya hili, bado lilikuwa na mkanganyiko.
“Mimi sijawahi kumuona kabla ya leo”
“Ok, haya basi tusubiri mgonjwa apate fahamu huenda akatueleza kilichotokea.. Lakini vipi ukiangalia hali yake, anaweza akazinduka kweli?” Aliuliza kwa shauku, alishakuwa na wasiwasi mkubwa juu ya huyu mzazi mwenzie, na muda huu ndio muda ambao alihitaji kuwa karibu zaidi na Khatib baada ya kuonyesha nia ya dhati ya kutaka kuwa nae.
“Tumuombe Mungu” Ndio maneno pekee aliyoweza kuyasema Dokta Iddi kwa wakati huu.
       ★★★★★★★★★★★★★★★★
Baada ya Hisham, Haroun na  Fred kuongoza msafara na kufanikiwa kufika Mbeya salama, hali ilikuwa tofauti na walivyoitarajia huko Mbeya. Wazazi wa Nira na wanaukoo wote waligoma kuupokea mwili wa marehemu Nira hadi hapo watakapomuona Khatib amekanyaga Mbeya. Hisham na Haroun walijitahidi kwa kadri ya uwezo wao kuwashawishi ndugu wa marehemu Nira lakini juhudi zao ziligonga mwamba.
“Wewe unajua huyo Khatib wakati anakuja hapa kwa mara ya kwanza alituambiaje?! Ni lazima aje yeye, hatuwezi kupokea maiti bila ya yeye kuwepo hapa” Alipigilia msumari wa mwisho Mzee mmoja aliyekuwa amevalia suruali nyeusi na koti kubwa jeusi huku ndani akivalia t-shirt nyeupe ambaye alijitambulisha kama Mzee Mwanachia.
Hisham ndiye aliyeonekana kuchanganyikiwa zaidi.. Akajaribu kupiga simu kwa Khatib, lakini haikupokelewa.
“Sasa tunafanyaje hapa kaka?” Hisham alimuuliza Haroun katika sintofahamu ile.
“Mimi sijui, maana nimejaribu kumpigia bosi hapokei”
“Tulishamjaribu mara zaidi ya ishirini tukiwa na Fred pale chini ya mti, hakupokea, sijui bosi ana tatizo gani kwakweli”. Alisisitiza Haroun ambaye aligundua kuwa Hisham hakuws akijua kuwa bosi wao hakuwa mwenye kupokea simu kwa muda mrefu sasa na si mara moja tu aliyomjaribu yeye.
“Hawa wazee watatufanya wajinga kaka, tugeuze tu na maiti yetu bana” Hisham aliongea kwa hasira. Haroun hakumjibu chochote alimwangalia kisha akatabasamu.
      ★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Mwanao amefariki, yupo Mochwari ya hospitali ya Bombo jijini Tanga” Alisema Mzee J4 baada ya simu yake kupokelewa. Mama Khatib alipigwa na butwaa, hakuamini hiki anachokisikia. Akakata simu haraka haraka na kuamua kumpigia mwanawe, simu yake haikupokelewa. Akapiga zaidi ya mara tatu katika simu yake ya dharura pia haikupokelewa. Akaamua kumpigia Hisham.
“Mbona rafiki yako hapokei simu, kuna tatizo lolote?”
“Ni muda mrefu sasa tunashangaa hata sisi mama, sijui nini tatizo” Hisham alijibu na kumfanya Mama Khatib azidi kuchanganyikiwa. Akakata simu ile haraka ili ampigie Sheikh Lesangwa.
“Haloo.. Samahani Sheikh Lesangwa ameuawa kikatili sana hapa nyumbani kwake” Ilisikika sauti ya upande wa pili baada ya simu yake kupokelewa. Akahisi kuchoka, mawazo mengi sana yakamzonga.
Akafikiria kwa dakika kadhaa..hakujua cha kufanya. Akamfuata Hawa aliyekuwa chumbani kwake amejipumzisha na kumuamsha.
“Tuko katika matatizo makubwa mwanangu, mimi naelekea Tanga muda huu, kuwa makini mpaka nitakaporudi, pesa za matumizi utaangalia katika ile pochi yangu ya pink iliyopo kule chumbani kwangu” Hakupoteza muda mama Khatib baada ya kuhakikisha Hawa ameamka.
“Mama nieleze kwa undani basi ni.....?”
“Nitakueleza mwanangu ngoja niende huko Tanga kwanza”. Alimkatiza na kugeuza kisha akaelekea alipoegesha gari yake, safari ya kuelekea Tanga ikaanza.
       ★★★★★★★★★★★★★★★★★
“No, that was not my intention (Hapana, hilo halikuwa kusudio langu)” Alikuwa akijitetea Sarah wakati anatoa maelezo katika kituo cha polisi kikuu cha Jijini Vancouver, Canada. Afisa polisi aliyekuwa akifanya nae mahojiano alishindwa kuamini maelezo ya Sarah kuwa hakuua kwa kukusudia.
          ★★★★★★★★★★★★★★★★★
Nini kitaendelea...??!!
Endelea kufuatilia.. Episode 030

Kama hujasoma episode za nyuma kuanzia 1 hadi 29 ni 'simple'... Bofya hapa>>>www.mdharubajk.blogspot.com

Jumanne, 16 Agosti 2016

HISTORIA BATILI 028

STORY: *HISTORIA BATILI*
MTUNZI: *Mdharuba, J.K.*
+255718274130
mdharuba@gmail.com
www.mdharubajk.blogspot.com
*EPISODE 028*
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
ILIPOISHIA...
Mzee J4 amemuibukia Khatib chumbani kwake katika hotel ambayo amefikia kwa ajili ya kutekeleza azma yake ya kumuua Mzee J4.

Sasa endeleaa....

“Huyu ameitupa hii simu ili apoteze ushahidi, sasa tuendelee kufuatilia magari yaendayo huku Iringa na Mbeya halafu tukafanye 'patrol' ya kueleweka huko mbele, tutamkamata tu mhalifu” Aliongea Afande Alfred kwa kujiamini huku akionesha kukasirishwa na kitendo walichofanyiwa na Hisham cha kuachwa solemba.
“Hapana afande, tutapoteza muda mwingi sana. Hiyo ni sawa na kusaka chaja ya 'smartphone' katika kijiji ambacho hata umeme hakuna.” Aliongea afande Mwita na kueka pozi, kisha akaendelea..
“Kwanza kati yetu hakuna anayemjua mhalifu kwa sura, bora tungekua na yule Regina mwenyewe hapa”.
“Afande mimi naona cha msingi ni kurudi kwenda kujipanga upya., huyu tumeshampoteza kwa leo” Alipigilia msumari wa mwisho Afande Omary na kusababisha wote wakapanda kwenye gari na kugeuza kurudi Morogoro mjini.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Khatib alishtuka sana baada ya kumuona Mzee J4 pale, hakutegemea!!. Aliishiwa nguvu, presha yake ikapanda kupita kiasi, akaanguka chini na kuzirai.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Walter, nini nitafanya mimi na hii mimba jamani na huku ni ugenini, nahisi kuchanganyikiwa Walter, nifanyeje?!” Sarah alikuwa akimlalamikia Walter huku akilia kwa nguvu sana. Alishindwa kuyazuia machozi mengi yaliyokuwa yakibubujika kwa wingi machoni pake.
Mapenzi yao yalikolea kiasi cha kujisahau kupita kiasi. Walikuwa wakifanya mapenzi pasipo kutumia kinga yoyote. Walijiachia sana bila kujua kuwa wapo ugenini tena wakiwa na deni kubwa la kusoma kwa bidii lililowatoa nyumbani kwao Tanzania na kuwapeleka nchini Canada kwa ajili ya masomo.
“Sarah nadhani unazijua vizuri sheria za chuo, hakuna mtu anayezuiwa kubeba mimba akiwa masomoni, sasa mimi sioni tatizo hapo zaidi ya kusubiria tu mtoto wetu”. Walter alionekana kutoshitushwa na jambo la Sarah kuwa mjamzito.
“Unamjua vizuri mtu anayenilipia ada hapa chuo Walter? Unamjua vizuri Mr Khatib wewe?” Sarah alishakuwa na hasira zisizo mithili, muda huu alishanyanyuka kutoka pale kitandani alipokuwa amekaa na kusimama huku akimwangalia Walter aliyekuwa amejilaza pale kitandani huku akiwa amekodoa macho katika 'Laptop' yake.
“Namjua vizuri yeye na mamaake kuliko unavyowajua wewe, lakini hawezi kuwa sababu ya kumchoropoa mtoto wangu aliyeko tumboni.”
“Kwahiyo Walter wewe ulikusudia kunipa mimba sio?” Majibu ya Walter hayakumridhisha Sarah.
“Nadhani wewe ndiye uliyekusudia nikupe mimba, maana wewe ndiye mwenye tumbo linalobeba mimba” Walter alishapandwa na hasira na yeye.
Jibu hili lilimfanya Sarah anyanyue glasi ya kioo iliyokuwa ipo katika meza ya mle chumbani na kumrushia Walter.
“Mamaaaaa... ” Alisikika Walter akipiga kelele za maumivu mara moja. Kisha kimya kikatawala huku damu nyingi zikimtoka kichwani.          ★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Nuro, Rukia, mimi nimewaita hapa tufanye kitu kimoja...” Ahmed alianzisha maongezi baada ya kuwaita katika kikao cha dharura maafisa wenzake.
“Tunakusikiliza” Detective Rukia ndiye aliyekuwa wa kwanza kuitikia.
“Nafahamu kuwa sisi tuna vyeo vidogo tu katika hii taasisi, lakini je, hii ndio itakua sababu ya sisi kuendelea kuwa wanyonge hadi dakika ya mwisho?” Ahmed alihoji huku akiwaangalia Rukia na Nuro kwa zamu. Wote walibaki kimya wakiashiria kuendelea kumsikiliza. Ahmed akaamua kuendelea...
“Sote ni mashahidi, nimefuatilia sana kuhusu Khatib, na kila mmoja ameona nini mkubwa wa kazi alichokifanya, sasa ni lini sisi tutaendelea kutumia kodi za wananchi katika kufuatilia mambo ambayo ripoti zake zinaishia kutupwa kapuni?!” Aliendelea kuhoji Ahmed akionesha uchungu wa kile wanachoendelea kufanyiwa na Ally Ngoswe mkubwa wao wa kazi.
“Ahmed hilo ni jambo la msingi sana uliloliongea leo, na nilitamani sana siku moja tuwe tunawaza sawa kama hivi.. Sasa katika hili, mimi nina wazo moja, nadhani litakuwa suluhisho la mambo yote”. Aliongea Nuro na kufanya Ahmed na Rukia wote wamkodolee macho kutaka kujua nini haswa anataka kuongea.
     ★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Wewe ni nani?” Aliuliza Sheikh Lesangwa baada ya kumuona ghafla mtu aliyeshika sime kali pasipo kujua ametokea wapi.
“Ismii Sayyeed.. Uriidu an uqatilaka (Jina langu Sayyeed nataka kukuua). Aliongea Sayyeed-jini rafiki wa Mzee J4 na kumfanya Lesangwa ahamaki.
“Kwanini uniue mimi sasa? Mimi nimekukosea nini? Mzee J4 ndiye aliyekuagiza?” Sheikh Lesangwa aliuliza maswali matatu mfululizo huku akitetemeka.
Sayyeed hakujibu chochote zaidi ya kunyanyua upanga na kutenganisha kichwa cha Sheikh Lesangwa na mwili wake.
“Japokuwa Mzee J4 hajaniagiza kufanya hivi, lakini naamini hizi zitakuwa habari njema akizisikia.” Aliwaza Sayyeed huku akitokomea na sime yake iliyojaa damu.
      ★★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Nimeletewa mgonjwa yuko hoi sana hapa, alipoteza fahamu, hana msaada lakini nahisi kama ni mtu unayemfahamu.. Naomba uje hospitali umtambue” Dokta Iddi Fauzi alisema mara tu baada ya simu yake aliyompigia Hamida kupokelewa.
“Sawa nakuja” Aliitika Hamida na kujinyanyua kutoka pale dukani na kwenda chumbani. Akavaa baibui lake na kuchukua pochi yake ndogo ya mkononi kisha akaenda moja kwa moja uani ambapo alimuaga mamaake.
“Mama, naenda hospitali mara moja, Dr Iddi amenambia kuna dharura..”
“Mmmh.. Leo hii.. Ni wewe au Hamida mwengine?, Dokta Iddi huyuhuyu uliyesema afuatilie wagonjwa na sio wewe? Mmmh haya kila la kheri, safari njema..”. Alistaajabu sana Nana kwa maelezo ya Hamida.
Hamida hakuongeza neno, akageuka na kutokomea.
“Hamidaaaa..umefunga duka wewe mtoto?” Nana aliita lakini Hamida alishapanda bodaboda wakati huu.
       ★★★★★★★★★★★★★★★★
Je, Nini kitaendelea?
Sarah na Walter?
Vipi Nuro ana wazo gani?
Khatib naye kimempata nini?
Je, kufa kwa Lesangwa ndio mwisho wa ufalme wa Khatib?

Usikose Episode 029

Kama hukusoma episode za nyuma.. Bofya hapa>>www.mdharubajk.blogspot.com

Jumapili, 17 Julai 2016

HISTORIA BATILI O27

STORY: *HISTORIA BATILI*
MTUNZI: *Mdharuba, J.K.*
+255718274130
mdharuba@gmail.com

www.mdharubajk.blogspot.com

         *EPISODE 027*
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
ILIPOISHIA...
Baada ya Khatib kutakiwa kuonana na Mzee J4 kabla ya saa sita mchana siku ya Jumanne, analazimika kuahirisha safari ya kumpeleka marehemu Nira kwa ajili ya kwenda kuzikwa nyumbani kwao Mbeya akiwa Mikumi.
Hii ni kutokana na maelekezo yaliyotoka kwa 'mtaalam' Sheikh Lesangwa.

Licha ya kuwa wanahisi Mzee J4 (ambaye anafuatwa na Khatib kwa ajili ya kuuliwa) hajui chochote, ndipo anapompigia simu na kumkaribisha Tanga na kumwambia "Nafurahi kuona unakuja kwa ajili yangu".

Je, nini kitaendelea...
Fuatana nami..

“Mama, Mzee J4 amenipigia simu na kuniambia eti nikaribie Tanga na anafurahi kuona naenda kwa ajili yake..” Alisema Khatib baada ya kumpigia mamaake.. Hii ni baada ya Mzee J4 kukata simu.
“Mmmh. Hebu jaribu kuwasiliana na Sheikh Lesangwa, mbona kazi imeshakuwa nzito hii..” Mama Mdharuba alisema kwa wasiwasi.
“Ok, ngoja nifanye hivyo..” Alimalizia Khatib na kukata simu. Kisha akampigia Sheikh Lesangwa.
“Aliyekupigia simu sio Mzee J4, ni jini lake tu linajaribu kukutisha, wewe fanya kama nilivyokuelekeza”. Aliongea Sheikh Lesangwa mara tu baada ya kupokea simu ya Khatib ilihali Khatib akiwa hajaongea chochote. Kisha akakata simu na kumuacha Khatib mdomo wazi na maswali mengi kichwani.
Akaamua kuzima simu yake na kuendesha gari moja kwa moja akielekea Tanga.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Hebu jaribu ku'track' gps ya huyo mpigaji” Alisema Afande Alfred kumwambia Koplo Mwita baada ya Hisham kukata simu aliyokuwa akiongea na Regina.
“Sawa Mkuu..” Aliitika Koplo Mwita na kuanza kulifanyia kazi aliloambiwa na Afande Alfred.
Kikapita kitambo cha dakika moja tu, Koplo Mwita wa kituo cha polisi kikuu cha Morogoro alimgeukia Afande Alfred na kumwambia..
“Anaonekana yuko maeneo ya Mikumi Afande”
“Andaa vijana wako haraka na mumfuatilie na kuhakikisha mnamtia mikononi mhalifu huyo” Aliagiza Afande Alfred.
“Sawa Mkuu” Koplo Mwita aliitika bila kuongeza neno.
Akatoka pale ndani ya kituo na kuwapanga vijana wake kisha wakajijaza kwende gari yao ya polisi aina ya LandCruiser kisha safari ya kuelekea Mikumi ikaanza.
“Afande mbona kama sio tukio la kawaida jinsi ulivyotutoa..?!” Aliuliza Afande Khamisi ambaye alikuwa ametii amri tu bila ya kujua makusudio ya safari hiyo ya ghafla.
“We unafikiri jitu linalotishia kuua bila uoga ni jitu la kuachiwa mwanya?” Alijibu kwa swali Afande Mwita licha ya kuwa swali lile lilielekezwa kwa Afande Omary ambaye ndiye alikua askari mwenye cheo cha juu kuliko wote mle garini.
Gari iliendeshwa kwa kasi sana kuelekea njia ya Iringa ili wafikie 'location' ambayo simu ya Hisham ilikua inaonekana ipo. Kadri walivyokua wakiendelea na safari ndivyo simu ya Hisham nayo ilivyokuwa ikionekana ikihama 'position'.
“Aisee.. Linaonekana linatembea hili jitu” Alisema Afande Mwita ambaye ndiye aliyekua ameshikilia 'GPS Tracker'.
Hakuna afande aliyeongeza neno, wote wakawa kimya huku gari ikiendelea na safari kwa kasi sana. Ni sauti ya mvumo wa upepo tu ndiyo iliyosikika.. Maafande wote watano waliokua wamepanda nyuma ya gari ile walikua wamesimama. Mbele ya gari akiwepo dereva na Afande Alfred ambaye mwanzoni alionekana kutoa amri kama ambaye hatokuwepo kwenye msafara kumbe naye alikua mwendaji. Walitembea kwa kasi kwa muda wa zaidi ya saa nzima, licha ya kuonekana kukaribia alipo Hisham, lakini GPS Tracker ilionesha Hisham anatembea mwendokasi wa kilometa 110 kwa saa, hivyo walitakiwa kuongeza spidi zaidi ili kuweza kumfikia.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Akiwa anaendelea na safari yake ya kuelekea Tanga, Khatib alihisi simu yake ambayo namba yake inajulikana na watu sita tu, akiwemo mama yake, inaita. Simu hii mara zote huwa haizimwi kwa ajili ya dharura za maana zaidi. Kwa kuwa simu yake aliamua kuizima, kuita kwa simu hii kunaashiria dharura kubwa sana.
Akaitoa mfukoni na kuiangalia kisha akapokea na kuweka sikio la kushoto huku akishikilia sukani ya gari kwa mkono wake wa kulia.
“Mama, kuna dharura gani?” Aliuliza mara tu baada ya kupokea simu.
“Umezima simu yako, mkuu wa kituo kikuu cha polisi Morogoro anakutafuta” Alisema mama yake na bila kuongeza neno lolote Khatib alikata simu.
Akawasha simu yake inayojulikana na watu wote, kisha akatafuta namba za Mkuu wa kituo kikuu cha polisi Morogoro na kumpigia.
“Ndio afande, nini kinaendelea..?” Alisema Khatib baada ya simu yake kupokelewa.
“Wasiliana na Hisham, vijana wangu wametoka kumfuatilia,punde tu watamkamata.” Alijibu Mkuu yule.
Kama kawaida yake Khatib hakuongeza neno, akakata na kumpigia simu Hisham.
“Bro, hao askari wanaokufuatilia wakikukamata basi utakuwa na madeni mawili kwangu, la Regina na hili la kuwekwa kituoni, yote yanasababishwa na udhaifu wako” Aliongea Khatib kwa hasira baada ya Hisham kupokea simu yake, kisha akakata simu na kuizima tena.
Hisham akabaki ameduwaa. Akazima simu yake kisha akatoa laini na kuitupa pembeni ya barabara ile simu. Huku akiwa bado katika spidi kali ya 110 km/hr.
“Wajinga sana hawa, watakua wanawasiliana na Regina. Ina maana Regina ameripoti kituoni?, mbona anataka mimi nizidi kuonekana mjinga? Ok, sawa.. Itafahamika tu” Alizongwa na mawazo Hisham baada ya kuitupa ile simu pembeni ya barabara.
“Haya kama wanafuatilia waache waendelee kufuatilia sasaa.. Pumbaaa.vuu” Alisema kwa sauti akifuatia msonyo licha ya kuwa alikua peke yake garini mle.
******************************
“Afande, linaonekana limesimama” Alisema Afande Mwita mara hii akimuonesha Afande Omary ile 'GPS Tracker'.
“Afande ongeza spidi huyu mtu tumemkaribia sana halafu amesimama” Afande Omary alitoa kichwa nje ya gari na kuchungulia pale alipo dereva huku akimwambia maneno hayo.
Gari ikaendeshwa kwa kasi kwa dakika kumi tu kisha Afande Mwita akasema wasimame.
“Kwanini tunasimama hapa porini wakati tuna zoezi muhimu?” Aliuliza afande Alfred.
“Ndipo alipo mhalifu”  Alijibu Afande Mwita akiwa ameshashuka kwenye gari huku ameshikilia ile 'GPS Tracker' akielekea pembezoni zaidi ya barabara kufuatia 'alarm' ambayo ilikua inapiga.
Askari wengine wote walishuka, garini akibaki dereva peke yake.
Afande Mwita alikifuatisha kifaa kile ndani ya dakika tatu ndipo alipoenda kuona simu ikiwa imetupwa ambayo hasa ndo ilikua 'location' wanayoitafuta.
“Shabaaash....” alisema afande Mwita na kuwashtua askari wote waliokuwa pale na kumkodolea macho.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Ndio nimefika Tanga hivi, niko katika hoteli moja hapa mjini, nitalala hapa..Nikumbushe kesho ni saa ngapi?” Khatib aliwasiliana na Sheikh Lesangwa baada ya kufika Tanga.
“Iwe kabla ya saa sita, ikiwa saa nne ndio vizuri zaidi” Alijibu Sheikh Lesangwa.
“Ok, nimekupata..” Alijibu Khatib na kukata simu.
Akavua nguo zake na kuchukua taulo alilopewa na muhudumu wa pale hoteli, na kujifunga kiunoni kisha akasukuma mlango wa kioo wa kuingilia bafuni. Alivyoingiza mguu wake wa kushoto na kutupa jicho ndani, akashtuka na kutaka kukimbia lakini akajikuta mzito na hawezi kujisukuma kwenda mbele wala kurudi nyuma.
“Usiogope, kesho saa 4 bado ni mbali sana, mimi nimeamua nije leo ili uniue mapema na uende ukaendelee na shughuli zako bwana Khatib” Alikuwa Mzee J4.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Je, nini kitaendelea? Askari watafanikiwa kumkamata Hisham?
Je, Khatib atafanikiwa kumuua Mzee J4? Au ni kipi kitaendelea?

Fuatana nami katika episode ya  028

Kama ulikosa episode ya 1 hadi 26 zisome hapa.. www.mdharubajk.blogspot.com

Whatsapp..
+255718274130

Jumatano, 30 Machi 2016

HISTORIA BATILI 026

STORY: HISTORIA BATILI
MTUNZI : Mdharuba, J.K.

        EPISODE 26
**********************
Pamoja na kuwa wamefika Mikumi wakiwa wanaelekea Mbeya, Hisham bado alikuwa na mawazo mengi sana juu ya hatma yake na uswahiba wake na Khatib utakuaje. Aliwaza sana na akakosa majibu ya maswali yake.. Alikua akiendesha gari kuelekea msibani lakini hana furaha hata kidogo. Mawazo mengi sana yalimzonga. Alifikiria endapo Regina ataamua kwenda kutoa siri anazozijua kuhusu yeye Hisham, akianzia alipomkuta mpaka hapo alipomuacha.. Pia alifikiria kama Regina ataamua kueleza kwa undani uswahiba halisi uliopo kati yake na Khatib, alihisi kuchanganyikiwa.
Akachukua simu yake na kujaribu kumtafuta Regina, pasi na kutarajia simu ikaita.. Akasubiri kwa sekunde kadhaa kisha akiwa katika hali ya mshangao zaidi, simu ikapokelewa.
"Halooo.. "
"Haloo, Hisham vipi mume wangu?" Aliongea Regina kwa kujiamini, huku simu yake ikiwa imeunganishwa moja kwa moja kituo cha polisi. Regina aliona ni busara kuliripoti hili jambo polisi mapema ili ikitokea amepata tishio lolote linalohatarisha maisha yake basi polisi wawe na taarifa.
"Uko wapi Regina?" Aliuliza Hisham kwa sauti ya umakini.
"Nipo tu, nini unahitaji kutoka kwangu?" Aliuliza Regina naye kwa kujiamini.
"Kwa sasa nahitaji roho yako, hicho ndio muhimu sana kwangu" Alishapanic Hisham kama kawaida yake. Yaani kwake kuulizwa anataka nini lilishakuwa kosa. Akaamua kuropoka hivyo pasi na kujua kuwa simu yake ilikua ikirekodiwa.
★★★★★★★★★★★★★★
Baada ya kukata simu ya mamaake, Khatib aliamua kupunguza mwendo na kuwasha taa ya pembeni inayoashiria kuwa anataka kuliegesha gari. Hii ikalazimisha magari yote yaliyokuwa nyuma ya msafara kupunguza mwendo na kutaka kujua ni nini haswa kinaendelea huko mbele. Wengine walishahisi labda tembo wa mbuga hii ya wanyama ya Mikumi wameshaziba njia kwahiyo wanatakiwa kusubiri.
Khatib alilazimisha gari zote zilizopo katika msafara ule ziegeshwe huku akimtaka Fred (ambaye ndiye alikua na gari yenye maiti) awaite wote waliokuwa katika msafara ule, ana jambo muhimu la kuwaeleza. Fred akatekeleza.
"Ndugu zangu nimewakusanya hapa kuna dharura imejitokeza, sitaweza kuendelea na msafara huu kwa leo, natakiwa nirudi Morogoro kisha niende Tanga leoleo" Aliongea huku akizungushazungusha kichwa chake kujaribu kuangalia kila aliyepo pale. Hisham ndiye alikua wa kwanza kujibu.
"Boss, nini kimetokea hicho muhimu kuliko msiba wa swahiba wako na mfanyakazi wako bora kwa miaka mingi?!"
"Iko nje ya uwezo wangu hiyo Mr. Hisham" Khatib alimjibu kwa ufupi na kumfanya akose swali la kuendeleza. Kisha Haroun ambaye kawaida yake sio muongeaji, anaongea pale panapohitajika tu, alionekana kutaka kuongea kitu.
"Kaka, kitu unachotaka kukifanya kitaleta matatizo makubwa, fahamu kuwa ni wewe pekee ndiye unayefahamiana na ndugu zake huko kwao. Ni wewe pekee ndiye unayepajua kwao. Wewe ni mtu muhimu kuliko sisi sote. Sisi tunaweza tukarudi sote na ukaenda peke yako na bado kukawa hakujaharibika jambo, lakini kukosekana kwako wewe mmoja tu hata tukienda sote bado hatujafanya kitu. Kwahyo naomba ufikirie mara mbili uamuzi wako". Haruna ambaye ni mkubwa sana kwa Khatib alijitahidi kumnasihi mdogo wake huyu huku akiweka heshima ya 'uboss' palepale.
"Kinachonipeleka Tanga ni muhimu sana kuliko hiki, Nira ameshakufa, kuna maisha yetu wengine lazima yaendelee... Na hatujui tumepangiwa kuishi miaka mingapi, kwahiyo hatuwezi kushughulika zaidi na Nira ambaye tayari ni marehemu halafu tukasahau ya kwetu sisi wazima" Khatib aliongea kwa kujiamini na kusababisha kila mmoja akiinamisha kichwa chini akiwaza jambo lake.
Kikapita kitambo cha sekunde zaidi ya 30 watu wote wakiwa kimya. Khatib akaamua kutoa hitimisho.
"Mimi nawatakia safari njema, mkazike salama, naomba kwa sasa Fred ndiye awe kiongozi wa msafara.. Nitampa namba za wahusika huko Mbeya mtawasiliana nao. Ningefurahi kuona wote mkiendelea na msafara ili mkaniwakilishe vema". Akaweka nukta kubwa kisha akamvuta Fred pembeni kidogo wakaongea kiasi cha dakika tano, kisha akarudi kwenye gari lake na kugeuza na kuanza safari ya Tanga moja kwa moja.
★★★★★★★★★★★★★
"Vipi umefikia wapi mwanangu?" Aliuliza Mama Mdharuba baada ya kupiga simu kwa mwanawe huyu wa kiume.
"Ndo nipo njiani narudi, nimewaacha waendelee na msafara".
"Sawa, umefanya maamuzi ya busara sana, kwahiyo unaenda Tanga moja kwa moja??!"
"Ndio, au ulitaka nipite hapo Dar una maelekezo ya ziada?!"
"Hapana mwanangu, wewe kaendelee tu na mambo yako, tutajuzana baada ya wewe kufika".
"Sawa mama, hakuna shida".
"Ila Sheikh Lesangwa anaweza kukupigia maana alinamboa kuwa atahitaji kuongea na wewe kidogo katika mambo ambayo mimi amekataa kunieleza" Mama Mdharuba alionekana kama kukumbuka kitu.
"Sawa akinipigia nitamsikiliza" Khatib alimjibu mama yake.
Na baada ya kupita dakika tatu tu tangu akate simu ya mamaake, bado akiwa njiani kuelekea Moro kisha Tanga, Sheikh Lesangwa alipiga simu.
"Bwana Khatib mimi sina mengi ya kuongea, bali nakutaka utakapofika Tanga usikutane na yule mamaake Abdul, nenda kwa ajili ya Mzee J4 tu.
"Sawa Sheikh nimekuelewa.." Aliitikia Khatib na kukata simu.
Akaendesha gari hadi Morogoro mjini, akapitia nyumbani kwake mara moja. Hii ikiwa ni pamoja na kuibeba bastola yake ambayo kwenyr safari ya Mbeya aliamua kuiacha.
Akaanza safari ya kuelekea Tanga.
Akiwa ameshafika mizani ya Mikese ambapo ni nje kidogo ya mji wa Morogoro, simu yake ikaita. Baada ya kuiangalia, mpigaji alikuwa ni Mzee J4.. Akafikiria kidogo kabla ya kuamua kupokea. Akapokea..
"Karibu sana Tanga, nafurahi kuona unakuja kwa ajili yangu". Alisema Mzee J4 na kukata simu.

Nini kitaendelea??!!
Usikose Episode 27

Je, Ulikosa HISTORIA BATILI Episode 1 hadi Episode 25?!!

Bofya hapa...
👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿
http://mdharubajk.blogspot.co.ke/?m=1

Jumatatu, 20 Julai 2015

HISTORIA BATILI O25

RIWAYA: HISTORIA BATILI (Fake History)
MTUNZI & MWANDISHI: JK
+255718274130
mdharuba@gmail.com

            EPISODE 025
              0⃣2⃣5⃣
★★★★★★★★★★★★★★★★
ILIPOISHIA....
Baada ya simu kukatwa, ndipo Khatib akagundua kuwa wenzake walishatangulia na amebaki peke yake, akawasha gari, akageuza na kuitoa kwenye maegesho ya Hotel na kuelekea msibani.
Wakati yupo barabarani akiendesha kwa kasi, kwa mbaalii akaanza kukumbuka maneno ya mama yake kuwa Mzee J4 alipaswa kushughulikiwa mapema.

SASA ENDELEA....
“Haloo.. Habari?”
“Safi tu”
“Habari za siku?”
“Nzuri”
“Ok, nilitaka kukusalimia”
“Nashukuru”
“Ok siku njema”
“Asante”
Baada ya kuona akijibiwa 'shortcut' sana, Dr Iddi aliamua kukata simu bila hata kuongea kile alichokikusudia. Hamida alishaanza kusahau kuhusu Dr Iddi, yeye mawazo yake yote yalikua kwa Khatib tu muda wote. Baada ya simu hii akamfuata mama yake aliyekua chumbani kwake akipanga nguo zake kabatini baada ya kuzianua.
“Mama, Dr Iddi kanipigia simu, sielewi anachotaka”.
“Mmmh, leo hii ndio huelewi anachotaka Dr Iddi? Kakufanyaje kwani jamani?” Nana alishangaa sana jinsi mtazamo wa Hamida ulivyobadilika.
“Mimi sitaki kumkwaza Khatib jamani, yule ni mzazi mwenzangu.. Sasa yeye Dr Iddi si ni mtu na mkewe? Kwanini aanze kunipigia simu kunisalimia? Sisi ndio wagonjwa tunatakiwa tuwatafute wao hao madaktari, lakini nashangaa mimi, Dokta ndo anawapigia simu wagonjwa... Hivi hana wagonjwa wa kuwahudumia huko?” Hamida alifoka.
“Usiseme hivyo mwanangu, kwani salamu inatia mimba?”
“Hata kama salamu haitii mimba mama, yeye anachotafuta kwangu ni nini?”
“Hivi Hamida umesahau jinsi Dokta Iddi alivyosaidi kuokoa maisha ya mwanao Abdul? Umesahau kweli?”
“Mimi hata sikujua kinachoendelea kuhusu Abdul siku ile, nyinyi ndio mlikuja kunambia kuwa eti sijui bila Dokta Iddi mtoto sijui angekufa sijui utumbo gani huko..”. Hamida aliongea na mama yake katika hali ambayo ilionyesha kuwa hapendezwi hata kidogo na jambo la Dokta Iddi.
“Mmh makubwa haya jamani, huyu Khatib kwakweli, sijui kakupa nini wewe mwanangu”.
“Mama, unavyotaka kuniaminisha kuwa mimi nilikosea kuzaa na Khatib ni jambo lisilokuwa zuri..na halina tija, yule ndio babaake Abdul, vyovyote vile iwavyo”.
“Sawa mwanangu, nimekuelewa mummy”. Nana aliona ni busara kufunga mjadala huu, maana huenda ukawa mrefu na kufikia pabaya.
★★★★★★★★★★★★★★★★
Lesangwa alifanya kazi kubwa sana na yenye mafanikio kwa upande wa Khatib na mamaake. Pesa aliyokuwa analipwa Lesangwa ilimtosha kufanya matumizi yake ya kila siku pasipo kuwa na shaka wala wasiwasi wowote na maisha. Alipewa pesa nyingi!!. Hizi zilimfanya awe mtumwa wa Mama Mdharuba ili asije akarubuniwa hata siku moja na kufanya mambo kinyume.
Mbali na pesa hizo, lakini pia alikuwa akisikilizwa sana katika shida zake zingine, tofauti na nje kabisa ya malipo ya kazi alizokuwa akizifanya.
Mtoto wake wa pekee aliyezaa na mke aliyenaye alisoma katika shule nzuri sana na ada akiwa analipa Mama Mdharuba. Hata gari analotembelea Lesangwa ilikua ni zawadi aliyopewa na Mama Mdharuba baada ya kumfanya kupata kiwanja kilichokuwa kinauzwa kwa shughuli za kibiashara licha ya kupambana na matajiri wakubwa zaidi waliokua na dau kubwa kumzidi. Yeye alifanikiwa kukipata kwa bei rahisi tena kwa haraka kupitia Lesangwa.
Lesangwa alikua na mchango mkubwa sana katika maisha aliyochagua kuishi Mama Mdharuba. Alimuheshimu mno, hii ni kutokana na kuwa hakuwahi kushindwa kazi yoyote kati ya zile alizotakiwa kuzifanya.
Kwa upande wake Lesangwa yeye hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuifanya kazi aliyokuwa anaambiwa kwa wakati, na vilevile alitoa ushauri kuhusu mambo yao kwa kadri mambo yalivyokuwa yakienda.
Jambo la Khatib kutofanya vile alivyokuwa anashauriwa na mamaake kwa ushauri alioutoa yeye Lesangwa, alishang'amua kuwa tayari kuna tatizo kubwa linakuja mbele yao.
Tatizo hili ambalo sababu kubwa ni Mzee J4, lingeleta taswira mbaya na kumuharibia sifa Lesangwa. Alishaona nini haswa Mzee J4 yalikua makusudio yake, na hatma ya mambo yatakavyokuwa endapo Mzee J4 ataachwa aendelee kama alivyo. Alimfahamu vizuri Mzee J4, na alijua nini kinampa kiburi. Ingawa kwa misingi na mipaka ya kazi yake, alikuwa hafanyi chochote mpaka aamrishwe kufanya hivyo na mabosi wake. Na hili ndilo sharti la wataalamu wote. Kufanya jambo bila kumwambia haliwezi kumuongezea yeye 'credit' kwani unaweza kuamini kuwa mambo hayo yametokea tu kwa bahati wakati si kweli. Kumwambia kisha akafanya na yakatokea, ndiko kunampandisha yeye na kuonekana anaweza mambo, hii inamsaidia kwa maslahi yake ya baadae.
Hivyo, Lesangwa alisubiri amri ya 'kudeal' na Mzee J4, lakini amri hii ilionekana kuchelewa mno. Aliona jinsi gani Khatib alivyokosea kumpa nafasi Mzee J4, na jinsi gani angemtesa..
Mzee J4 kupitia jini wake Sayyeed alijitahidi sana kutafuta nani haswa aliyekuwa nyuma ya Khatib na mamaake katika upande huu wa ulimwengu usioonekana, lakini alifeli.!! Kufeli huku kulitokana na jinsi Lesangwa alivyokuwa amejidhatiti na kujiwekea ulinzi mzito wa kutoonekana kirahisi na maadui. Hali hii ilimpa tabu Mzee J4 kwani aliamini kwa namna moja ama nyingine ni LAZIMA watu hawa wangekuwa wanajihusisha tu na mambo haya. Lakini kwa nini Sayyeed anashindwa kung'amua?!..
Hii vita tayari Lesangwa alishaifahamu, lakini aliamua kusubiri 'outcome'.
*************************
“Haloo Mama, nipo msibani, Nira, yule aliyekua akisimamia pale yard amefariki. Kwahiyo ndio tupo katika taratibu za awali za maziko kabla ya kuupeleka mwili wa marehemu Mbeya kwa ajili ya mazishi”. Khatib alimpigia simu mamaake kumjulisha kinachoendelea.
“Sawa mwanangu, poleni sana na kila la kheri huko”.
“Ok, sawa mama Ahsante, ila kabla sijasahau naomba uongee na Sheikh Lesangwa umwambie ampunguze kasi Mzee J4, ameshakuwa tatizo”.
“Mzee J4 ni tatizo tangu mwanzoni, mimi nilimuona, sema wewe mwanangu saa zingine unakuwa mbishi kama shipa, sasa hapo yameshakutokea puani ndo unanambia nimtafute Lesangwa, wewe si uliamua kumkumbatia?”. Mama Mdharuba aliamua kumshambulia mwanawe baada ya kuelezwa kuhusu Mzee J4.
“Mama, niko msibani kama nilivyokwambia, kwahiyo nadhani huu ni wakati wa utekelezaji zaidi kuliko lawama. Naomba weka pembeni lawama kwa sasa, tu'solve' hili kwanza halafu uta'resume' lawama zako baadae.”. Khatib aliongea sentensi za kibabe katika hali ya ustaarabu.
“Sawa, ngoja nifanye hivyo, nitakutafuta baadae..”. Mama Mdharuba aliaga na kukata simu ili moja kwa moja amtafute Lesangwa.
★★★★★★★★★★★★★★★★
Hisham ndiye mtu pekee aliyekuwa pale msibani na huzuni kuliko watu wote. Marehemu huyu kwenye kichwa cha Hisham alionekana ni mtu anaeenda kuyavuruga kabisa maisha ya Hisham.
Mlolongo wa mambo yote yatakavyoenda kitovu chake ni Nira.
Nira ndiye mtu aliyemwambukiza Regina Ukimwi, mwanamke aliyempenda na kuishi nae kwa miaka mingi. Kupitia Ukimwi huu ambao Nira ameupandikiza mwilini mwa Regina, umesababisha Regina atoroke. Kutoroka kwa Regina kunampa uhusiano mbovu na swahiba wake Khatib, na huenda pengine akaamua kumporomosha au kumuua kabisa kwa kushindwa kumuua Regina. Hili litapelekea maisha yake kuvurugika kabisa.
Mara nyingi Hisham amejikuta akizinduliwa kutoka katika dimbwi la mawazo wakati watu wakiwa katika mipango ya maziko ya Nira. Na hii ilichangiwa zaidi na sentensi ya Khatib mara tu baada ya kufika pale msibani, kwani alimuita Hisham na kumnong'oneza “Tutaongea baadae kuhusu jambo letu, hapa tuangalie msiba kwanza.. Ila jambo la Regina kutoroka HALIVUMILIKI”.
Neno HALIVUMILIKI lilikuwa likijirudia sana kichwani mwa Hisham na kumfanya azidi kuwa na mawazo muda wote.
HALIVUMILIKI ilikuwa haitafsiriki.
"Ni kwa kiasi gani hili jambo litakua halivumiliki kwa Khatib?" Ndilo swali lililokuwa kichwani mwa Hisham wakati wote. Alimfahamu vizuri Khatib kuwa ni mpole mbele ya macho ya watu tu-lakini sio uhalisia wake. Khatib ni muuaji, tena katili haswa ambaye kutoa roho ya mtu kwake lilikua jambo la kawaida sana.
“Bro, maiti hii lazima isafirishwe leo kwenda Mbeya, kwahiyo changamka ili tukamilishe utaratibu hapa haraka tuanze safari, naona una mawazo sana ndugu yangu, sijui tatizo ni nini?!” Haroun alivunja ukimya huku akiwa amemshika mkono Hisham aliyekuwa ameegemea nguzo ya turubai lililokuwa msibani hapo akimtaka atoe ushirikiano.
“Kazi niliyopangiwa na boss nimeikamilisha mapema tu kaka, labda wewe unataka nifanye nini?”. Hisham alimkodolea macho Haroun.
“Ok, sawa lakini unaonekana hauko sawa kaka, tatizo ni nini?” Haroun aliuliza
“Niko poa Haroun, kawaida tu.. Nahisi kama kijihoma kinaninyemelea”. Aliamua kudanganya.
“Ok, pole sana, maana nakuona umenyongea sana”.
“Ahsante sana bro”.

Baada ya mipango yote kukamilka, safari ya kuelekea Mbeya ikaanza mara moja, Khatib hakutaka kabisa waucheleweshe mwili ule kwa ajili ya mazishi. Pia alitaka ndugu zake Nira wapate kupata muda wa kutosha kuuaga mwili wa ndugu yao kabla ya kuuzika. Hivyo safari ya kwenda Mbeya ikaanza jioni ile ya saa 11. Hisham, Khatib na Haroun kila mmoja akiwa katika gari yake peke yake. Fred alikuwa katika Canter ndogo ambayo ndiyo ilibeba mwili wa marehemu. Huku ndugu na jamaa wengine wakiwa katika usafiri wao binafsi na wengine wakiwa katika 'Coaster mayai' mbili ambazo Khatib alizikodi. Gari ya Khatib ikitangulia mbele kwani ni yeye pekee ndiye alikuwa akipajua nyumbani kwa kina Nira. Ikafuatia gari yenye maiti, kisha ikafuatia ya Hisham, na ya Haroun na gari zingine ndogo nne, zikifuatiwa na zile Coaster mbili, safari ikaendelea.
**************************
“Khatib,uko wapi mwanangu?” Neno la kwanza la Mama Mdharuba baada ya simu yake kupokelewa na Khatib licha ya kuita muda mrefu sana.
“Niko Mikumi, ndio tunaelekea Mbeya hivi kwa ajili ya kuuzika mwili wa Nira”. Khatib alimjibu.
“Lini mtarudi huko?” Mama Mdharuba aliuliza kwa shauku.
“Ni mpaka tuuzike huu mwili, nadhani baada ya siku tatu.. Leo ni jumatatu kwahyo nafikiri kwenye Ijumaa hivi ndo tutakuwa tunarudi huko”. Khatib alitoa majibu kwa makadirio licha ya kuwa hajafika huko msibani na kuona hali itakuaje.
“Duuh, sasa ni hivii...” Mama Mdharuba alionekana kushangaa ratiba hii ngumu kwake.
“Enheee..nambie mama” Khatib aliitikia kutaka kujua mama yake anataka kusema nini!!.
“Ndio nimetoka kuongea na Lesangwa hapa, yeye amenambia kuwa unatakiwa uonane na Mzee J4 Tanga kesho Jumanne kabla ya saa saba mchana, ndio siku nzuri ya kumpatia pekee, kinyume na hapo HAIWEZEKANI tena na atatuathiri sana..kwahiyo nakuomba ufanye juu chini kuhakikisha kuwa unaahirisha hiyo safari ili ufanye hili la msingi kwanza..” Mama Mdharuba aliweka nukta ndogo kusikiliza Khatib atasema nini.
“oooohpsss... Daaaah..yaani hapo tu ndo tunapogombana mimi na nyinyi, mambo yenu mnapanga muda kama vile mimi sina shughuli zingine za kufanya..!! Angalia sasa..!!”. Khatib alimtupia lawama mamaake.
“Mwanangu, hizi zote ni juhudi zangu kuhakikisha kuwa 'status' yako haishuki, Lesangwa mwenyewe nimefanya kumbembeleza tu kwa sababu mwanzo ulishaonyesha kudharau.. Kwahyo hiyari unayo mwenyewe, kama utaenda kumzika Nira au utaenda kulinda status yako..kazi kwako, viwili vinachagulika”.
★★★★★★★★★★★★★★★★★

”Kila mtu ana matatizo, na huenda matatizo yako wewe kwa sababu ya kukosa pesa ni madogo zaidi kuliko ya yule mwenye pesa... RIDHIKA..” Mdharuba JK.

Tukutane Episode 26.

Jiandae kusoma kitabu, siku ni chache zimebaki ili kitoke.

Maoni: mdharuba@gmail.com
+255718274130

Alhamisi, 16 Julai 2015

HISTORIA BATILI O24

RIWAYA: HISTORIA BATILI
MTUNZI: Mdharuba JK
+255718274130
+255654727266

           EPISODE O24
               2⃣4⃣
★★★★★★★★★★★★★★★
ILIPOISHIA..
“Sawa kaka nimekupata, wewe nipe huu usiku halafu utaona”. Hishan aliitikia huku mwili ukimtetemeka.
“Poa, ila nakukumbusha tu kuwa ukiua kwa bastola ujue jela itakuhusu, sitakuwa na msaada kwako”. Mr Khatib alimalizia na kukata simu.
SASA ENDELEA...
Pamoja na shinikizo hili la kumuua Regina, Hisham alianza kumfikiria Regina kwa upande wa pili kama ambavyo alikua akiishi naye kwa kipindi cha miaka zaidi ya saba!
Alipata tabu sana kimawazo. Regina ndiye alikua mwanamke pekee ambaye alimjua vizuri Hisham, alimfariji, alimshauri, alimvumilia, alikuwa nae bega kwa bega tangu kipindi ambacho hana kitu mpaka leo akiwa ana maisha mazuri sana.
Hisham alikumbuka pia mara ya kwanza kukutana na Regina, akiwa amelewa 'chakari', hajitambui.. Regina alimsaidia.
Kilichokua kinamsumbua Hisham ni kuona kuwa anamuua Regina kwa sababu moja tu ambayo ni kulinda maslahi yake yeye na Khatib, lakini hakuwa na ubaya wowote katika nafsi yake.
Regina alikuwa mtu muhimu sana kwake, lakini alimfikiria rafiki yake Khatib, ambaye akienda kinyume na matakwa yake angekosa ushirikiano naye, na pengine hata angemuua!! Kichwa kilianza kumuuma..
Wakati yuko katika dimbwi hili zito la mawazo, ujumbe mfupi uliingia katika simu yake, akafungua na kuanza kuusoma..
“ Kaka, najua kinachokusumbua mpaka sasa ni kufikiria wema aliokutendea huyo mwanamke hadi leo, lakini unasahau kuwa huyo tayari ni mwathirika, alikusaliti, na angekuambukiza UKIMWI, sasa sijui ni kipi haswa kinakufanya usite kumuondoa, fanya maamuzi sahihi, wewe ni Jemedari wangu mkuu na nakutegemea sana kaka”..
Ujumbe huu ulimpa Hisham nguvu mpya na kunyanyuka pale alipo moja kwa moja akaelekea chumbani kwake.
Alimkuta Regina bado hajalala, akiangaza huku na huko mle chumbani.
“Mke wangu, mbona unaonekana kuwa na mawazo sana? Tatizo kubwa ni nini? Mimi sina kinyongo na wewe, na hya yote nimeshayasamehe, mbona unaonekana unashindwa kulala?”
“Hisham, najisikia vibaya sana, naomba unifungulie mlango nitoke nje kule kwenye bustani nikapunge upepo”.
“Ukapunge upepo usiku huu?”
“Ndio mume wangu, yanipasa kufanya hivyo kwa jinsi ninavyojisikia”
“Ok, sawa.. Twende pamoja”.
Hisham akafungua milango ya nyumba ile na kutoka na Regina mpaka katika bustani nzuri ya nyumba ile, sehemu waliyoweka maalum kwa ajili ya kupumzikia. Walijengea kibanda kidogo cha makuti na mabenchi ya mbao na meza vilivyochongeshwa kwa umaridadi mkubwa sana. Hapa palipendeza sana.
“Pole sana mke wangu, matatizo ni sehemu ya maisha, usihuzunike sana”. Hisham alijitahidi kumliwaza mkewe ili kumuonyesha kuwa yuko pamoja nae katika hali yoyote ile iwayo.
Kwa Regina kulikuwa na wazo tofauti, hakumuani Hisham hata kidogo, hapa alimwingiza katika mtego huu ambao alikua anaomba Mungu uende sawa.
“Natamani nipate juisi ya bariidiii..nipoze koo mume wangu” Regina aliongea baada ya mazungumzo ya muda mfupi.
“Kwahiyo unataka kuniambia kuwa unanituma niende ndani nikakuchukulie juisi?” Hisham aliongea huku akitabasamu.
“Yaah, mume wangu, nani mwengine wa kumtuma zaidi yako?” Regina aliongea naye akionyesha tabasamu lake kwa mara ya kwanza tangu asubuhi.
Hii ilimfanya Hisham aone kuwa sasa anakaribia kumteka Regina. Akachomoka mbio kuelekea ndani kwenye friji na kuchukua juisi.
Kwa Regina huu ndio muda aliokuwa akiusubiri.
Kiasi cha pesa ambacho alichukua mle ndani wakati Hisham akiwa sebuleni na kushindilia kwenye nguo yake ya ndani na zingine kwenye sidiria, aliamini kitaweza kumfikisha aendako salama.
Zilipita dakika tatu tu Hisham akarudi pale alipokuwa amekaa na mkewe, ila alishangaa kwa kuwa Regina hakuwepo eneo lile. Akaangaza huku na huko, bado Regina hakuonekana, akaanza kuita huku akizunguka maeneo mbalimbali ya nyumba ile lakini bado hakufanikiwa kumuona Regina!!. Akalielekea geti la nyumba ile na kufungua na kutoka nje huku bado akiendelea kuita bila mafanikio.
★★★★★★★★★★★★★★★★
“Inakuaje mama Mdharuba anakua sababu ya kifo cha mamaako?” Sarah alimuuliza Walter kwa hamaki kubwa akiwa haamini anachokisikia kutoka mdomoni mwa Walter.
“Mamaangu aliwahi kushiriki biashara na mama Mdharuba, miaka ya nyuma enzi ambazo mimi nilikua mdogo sana, ni baba ndiye aliyenieleza stori hiyo”. Walter alianza kufunguka.
“Enzi hizo bado Mama Mdharuba hajakuwa vile alivyo sasa, yaani namaanisha kuwa mwanawe bado alikua hajapata pesa zile alizonazo sasa..”
“Walter, unataka kunambia kuwa Mr Khatib hakurithi mali za babaake kama tunavyojua?”
“Pole mno Sarah,  yeetoh wejungulukwe ni kivwiri kibaha, kila upande wa mwiri wako kiathi ambacho kikugera kija mwaaka wethidhona  handu weelekea,,,harika uhana bahati mbivi mno hamwe naiti wethina ikotha (Pole sana Sarah, umezungukwa na kivuli kikubwa kila upande wa mwili wako, kivuli hiki kinakufanya uone giza kabisa na kutojua unakoelekea, wewe ni katika watu wenye bahati mbaya sana ingawa huna kosa). Walter aliongea kwa kipare kuweka msisitizo juu ya anachokiongea.
“Walter unaongea kwa mafumbo sana, nashindwa kukuelewa mylv”.
“Stori iko hivii... khatib na mama yake walikuwa watu maskini sana huko nyuma, hizi habari kuwa amerithi mali si za kweli, ila yapo waliyoyafanya..ila mimi sitakuambia lolote maana ukimchunguza bata utashindwa kumla..
Mama yake alishirikiana na mama biashara flani kipindi hcho, na baada ya kuwa wanaelekea kupata mafanikio makubwa, mama Mdharuba alifanya njia zake za kishirikina kama kawaida yake ili amzuge mama apate kumdhulumu, Mama hakukubali, ndipo akaamua na yeye kupambana. Ila hakujua kuwa mpambano huu alikua na nafasi ndogo sana ya kushinda,, angejua hivyo, angeacha, kuliko kutuacha sisi wapweke tukiwa bado wadogo sana. Kwahiyo mimi nikisikia kuhusu Mama Mdharuba nakumbuka tu mama yangu alivyofariki,.. Ila Sarah, sipendi kuongelea hili jambo tena, kwahiyo nakuomba usiniulize hata swali moja baada ya maelezo haya”.
“Ok, sawa baby, nimekuelewa”. Sarah aliitikia kinyonge ingawa alitaka kufahamu zaidi, hapa mawazo juu ya Khatib yalishabadilika.
★★★★★★★★★★★★★★★★
Sasa ni majira ya saa tatu asubuhi, Mr Khatib akiisubiri kwa hamu simu ya Hisham, hatimaye simu yake ikaita, ila tofauti na alivyotarajia, mpigaji alikua Fred..
“Haloo, Fred vipi? Kwema?”
“Hapana, sio kwema boss”
“Nini tatizo tena?”
“Nimepata taarifa kuwa Nira amefariki muda huu, kwahiyo nilitaka nikujulishe kuwa nitafunga ofisi ili tuweze kuhudhuria huko msibani ili tuone taratibu za mazishi zinaendaje..”
“Oooh, ok, kumbe Nira amefariki..sawa.. Nadhani tutakutana huko haina shida”
“Ok, sawa boss”.
Baada ya kukata simu hii alimpigia simu Hisham,
“Mume mwenzako amefariki bwana Hisham”. Ndivyo alivyoongea Khatib baada tu ya salamu.
“Nani tena?! Nira au?” Hisham aliuliza kana kwamba hajui kuwa Mr Khatib alimaanisha nani.
“Yaah, fanya twende msibani, maana najua kazi ya kumpoteza Regina imekushinda”.
“Kaka wee acha tu, yule mwanamke kanitoroka jana usiku bana..”. Hisham alilalama akiwa anaamini Khatib hajui kinachoendelea.
“Pole sana, nilipewa taarifa leo asubuhi kuwa alionekana akitumia usafiri wa lori kuelekea kwao, nikajua tayari amekutoroka huyo, hakuna namna nyingine hapo”. Mr Khatib aliongea maneno ya kweli yaliyoashiria kuwa alikua na mtandao mrefu sana na kumfanya Hisham ajione bwege kwa kutomdhibiti Regina pale kwake.
“Kwahiyo unataka kunambia unajua anapoelekea?”. Hisham aliuliza swali hili ili ikiwezekana aanze kumfuatilia Regina na kufuta uzembe ambao ameonekana anao.
“Njoo tukutane Euler Hotel hapa tumchukue na Haroun tuelekee msibani, tutayaongea huko”. Khatib alimjibu Hisham na kukata simu.
“Sawa boss” Hisham aliitikia lakini simu ilishakatwa.
Wakakutana Euler Hotel wakajadili jinsi gani wataonyesha kuguswa na msiba ule na waubebe kama wao.
Hilo lilikua jambo la msingi sana kwao kuweka sawa 'status' zao kwenye macho ya watu. Licha ya kuwa vitu vingi anavyomilikia Khatib havikujulikana, lakini yard yake ikijulikana na kila mtu, na kila mmoja alijua kuwa Nira ndiye alimuajiri kuwa mkurugenzi wa pale. Hivyo watu wote wangetegemea kumuona Khatib akishiriki kikamilifu kwenye msiba ule.
“Haroun wewe nakukabidhi sekta ya vinywaji pale, hakikisha kwenye msiba huu watu hawakaukiwi maji kabisa, kama na soda zitakuwepo pia itakua poa sana.. Hisham utanisaidia kunitengenezea mandhari nzuri ya watakaokuja msibani, hakikisha hakuna mtu anakosa kiti, halafu pia ushughulike na masuala ya usafiri ili tuupeleke huu mwili kwao Mbeya kwa ajili ya kuzikwa, mimi niachieni suala la chakula, nitalimaliza mwenyewe, na kama nitahitaji msaada wenu nitawaambia..”. Mr Khatib alimaliza kugawa majukumu na kuweka sawa kila kitu kabla hawajafika eneo la tukio. Kutangulia kwa Fred eneo lile kuliwapa nafasi ya kujipanga kwani Fred anaweza kutuliza presha ile ya msiba iliyopo pale huku wakisubiri vigogo hawa ili waweze kuendesha msiba vizuri.
“Ok, sawa boss hakuna shaka” Aliongea Haroun ambaye muda mrefu sana alikua kimya.
Wakatoka hotelini pale na kuelekea kwenye magari yao na kila mmoja akazama kwenye gari yake tayari kwa safari ya kuelekea ulipo msiba.
Baada tu ya kuchomeka ufunguo, Kabla hajawasha gari yake, Khatib alisikia simu yake iliyokua mfukoni iki'vibrate' na kutoa mlio kuashiria kuna sms imeingia. Akaitoa mfukoni, na kusoma sms ile ambayo ilionekana kutoka kwa Mzee J4, ilikua na neno moja tu "NIPIGIE". Kitendo hiki kilimfanya Khatib asijiulize maswali mengi, moja kwa moja akampigia Mzee J4 kumsikiliza anasemaje.
“Ndio Mzee, Habari ya leo?”
“Niko salama tu kijana wangu, pole sana kwa kumpoteza Jemedari wako muhimu bwana Nira”.
“Asante sana, nimeshapoa mzee..taarifa hizi umezipata tayari? Maana msiba umetokea muda sio mrefu, na sijaanza bado kusambaza taarifa”. Khatib aliuliza kwa hamaki kanakwamba amemsahau Mzee J4.
“Hilo sio la msingi kwa sasa, ila nataka nikupe pole zaidi kwa kushindwa kufanikisha mpango wako haramu wa kumshawishi Hisham kumuua mkewe-Regina”. Khatib aliishiwa nguvu ghafla, hakuwa na la kuongea zaidi ya kumuacha Mzee J4 aendelee.
“Nadhani umesahau kuwa uliniahidi utaachana na haya mauaji, bado unaendelea, nilikuambia usinikere, nahisi umesahau licha ya kuwa uliniahidi kuwa hutonikera. Bado unafikiria kuwa kuua ni njia sahihi zaidi kwako,, nakupa onyo kwa mara ya mwisho”. Mzee J4 alionekana kuchukizwa sana, na baada tu ya maneno haya alikata simu.
Baada ya simu kukatwa, ndipo Khatib akagundua kuwa wenzake walishatangulia na amebaki peke yake, akawasha gari, akageuza na kuitoa kwenye maegesho ya Hotel na kuelekea msibani.
Wakati yupo barabarani akiendesha kwa kasi, kwa mbaalii akaanza kukumbuka maneno ya mama yake kuwa Mzee J4 alipaswa kushughulikiwa mapema.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Mzee J4, Mama Mdharuba, Hisham, Walter, Sarah... Kila mmoja anasababisha tatizo lake kwa mtu mmoja tu, Mr Khatib!! Pesa ina matatizo mengi sana.

Dont Miss Episode 25

Nimerudi kama ifuatavyo...

Maoni: mdharuba@gmail.com
+255718274130

Kitabu kinakuja, jiandae kununua..!!.

Ijumaa, 12 Juni 2015

HISTORIA BATILI O22

RIWAYA: Historia Batili (Fake History)
MTUNZI: Jumaa Khatib Mdharuba (Jk)
     +255718274130

         EPISODE O22
★★★★★★★★★★★★★★★★
ILIPOISHIA..
Mzee J4 anataka kumpa ushauri Khatib apate cha kufanya na kujiepusha na mauaji anayoendelea nayo.
Huku nako Dr Mwinyi anampigia simu Hisham kutaka kujua kama tayari amekamilisha mauaji ili watengeneze ushahidi haraka, hii ni baada ya Dr Mwinyi kupigiwa simu na Khatib na kupewa maelekezo.

SASA ENDELEAA..
Baada ya kukosa cha kumjibu Dr Mwinyi,Hisham alikata simu. Regina, pamoja na mawazo tele aliyokuwa nayo kichwani kwake, aliigundua ile simu aliyoipokea mumewe kuwa ilimuhusu kwa namna moja au nyingine. Pamoja na kufarijiwa sana na Hisham mpaka akaamua kubaki pale, lakini wasiwasi juu ya hatma ya maisha yake ulikua mkubwa.. Alimfuatilia vizuri Hisham tangu anapokea simu, na jinsi alivyogeuka kumuangalia kabla ya kukata simu. Akahisi kuna jambo. Bahati nzuri Regina alipata kufahamu vitu vingi kuhusu Khatib kupitia mumewe-Hisham. Hivyo alifahamu kuwa kama jambo lake la kukutwa na HIV atashirikishwa Khatib, kulikua hakuna namna nyingine zaidi ya yeye kuuwawa..na kwa jinsi pia anavyofahamu uhusiano wa Hisham na Khatib ulivyo, aliamini kuwa mpaka sasa Khatib ana taarifa zake. Hata hapa aliposikia mumewe akitaja neno Dokta, alijua kuwa tayari 'kimenuka'. Hapa akili yake iliwaza kitu kimoja tu-Kutoroka.. Alishapanga kutolala nyumba hii leo, ingawa kichwa chake kiliuma kwani hakujua angetoka vipi pale.
“Nini tatizo mume wangu? Mbona unaonekana umeduwaa halafu umekata simu?” Regina aliamua kusikiliza jibu la Hisham kwa swali hili.
“Huyu Dokta nilikua na ahadi, nilipanga tukapime kwake, lakini sikwenda huko..ndo ananiuliza hivi maana nilimuahidi nitaenda nimkute, sasa kaona kimya” Hisham alidanganya, na kumfanya Regina awe na maswali mengi zaidi..
“Sasa kwanini umemkatia  simu? Si ungemwambia ukweli tu kuwa tumeshapima hospitali nyingine?” Alichokuwa akikifanya Regina hapa ni kuendelea kupata ukweli tu kuwa kuna mpango maalum, na kwakuwa alimfahamu vizuri Hisham kuwa mara nyingi ni mwepesi wa kupanic akiambiwa ukweli, aliamua kukazia msumari.
“Nimekata ndio, kwani we huoni kuwa nimechanganyikiwa? Sasa nitamueleza nini yeye? Hebu achana na hizi habari za Dokta, kwanza simu si nimepigiwa mimi? Wewe mbona maswali mengi?”  Hisham alipandisha sauti na kumfanya Regina ajue nini kinaendelea hapa.
“Basi mume wangu, samahani sana” Regina aliamua kuwa mpole.
Alilala pale kitandani na mawazo meengi sanaa.. Alijua kuwa Hisham leo hatatoka kwenda kazini kama kawaida yake, hilo alilifahamu kwani ni lazima Hisham atakua na mpango wa kumuua tu.
Hisham yeye alikuwa akiusubiri kwa hamu usiku wa leo, ili Regina atakapolala tu, ampake ile sumu ya unga maeneo ya puani ili ndani ya dakika 10 asiwe miongoni mwa watu hai wanaoishi duniani.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Labda niwaulize swali moja muhimu, hivi mnafikiri nyinyi ni nani katika nchi hii?” Ally Ngoswe alikuwa amewatolea macho Detective Rukia na Ahmed Khamis baada ya kuwaita ofisini kwake. Licha ya kuwa alishirikiana kwa karibu sana na Noor, ila Ally Ngoswe alipinga wazo la Noor na Khatib kutaka kumuua Ahmed. Aliamini kwa kumuua Ahmed mambo yangevurugika zaidi katika idara hiyo, na huenda Ngoswe angebeba mzigo mkubwa wa lawama ambao ungeambatana na uchunguzi mzito. Na kwakuwa alishamuonyesha Detective Rukia wazi kuwa alipinga jambo la Ahmed kwenda Canada wakati ni jambo liliokuwa likifanywa ndani ya misingi ya kiusalama, hivyo kuruhusu kufikia huko kwenye uchunguzi kungefanya yakaibuka mengi zaidi..
“Naomba tusamehe mkuu, hili kosa ni kubwa tumelifanya, tulidhani tukishakamilisha itakua bora zaidi kukufahamisha. Ila sisi tunakiri tumekosea, na tunakuahidi kosa halitojirudia mkuu” Rukia alijitetea kwa niaba yao wawili.
“Sitaruhusu ujinga huu ujitokeze tena, na kuanzia sasa hiyo kesi ya Khatib naitoa mikononi mwenu, na nitaikabidhi kwa wengine.. Na Ahmed urudi kule shule ukawaage, tutatengeneza uhamisho ndani ya wiki moja urudi hapa nijue nitakupanga wapi, Detective nitakupangia kazi nyingine mbali na hii. Halafu naomba ripoti ya Nuro nijue nae namkabidhi jukumu lipi, ingawa yeye ataendelea kubaki kulekule.. Sihitaji maelezo mengine ya ziada..hii ni Command!” Ally Ngoswe ndivyo alivyomaliza na kuwaonyesha ishara wawili wale watoke nje.
Ahmed na Rukia walitoka nje ya ofisi ile huku wameinamisha vichwa vyao, hawakujua sababu haswa ya 'boss' wao kuamua vile. Wakaanza kuhisi kuna mchezo mchafu nyuma yao. Rukia akatoa simu yake katika pochi yake ndogo ya rangi ya pink aliyokuwa ameshikilia mkononi, akaamua kumpigia Nuro huku akitembea kurudi ofisini kwake.
“Mwenzangu, leo wenzako tumebadilishwa vitengo na boss..tumetolewa kwenye hiyo 'case' ya Khatib” Rukia aliongea baada ya salamu.
“Yaah, nililitegemea hilo tangu ile siku ulivyonambia 'boss' alikuita ofisini na kukuuliza kuhusu Ahmed..” Nuro hakuonekana kushtushwa na hii habari, ila akaamua kumpa Rukia habari zingine ambazo hakuzifahamu kabisa..
“Unajua mimi nafahamiana sana na Noor, yaani ni mtu wangu wa karibu haswa, yeye ndiye aliyenitafuta na kuniambia nimtafutie Khatib mke, yaani nina maelewano naye mazuri sana tangu zamani, nikipata siku ntakueleza nilifahamiana nae vipi, ila mpaka leo yeye hajui kuwa mimi ni Usalama” Maelezo haya yalimfumbua macho Rukia, ila alikua hajapata mwanga haswa Noor anahusika vipi katika 'issue' ya boss Ally, akaamua kuendelea kusikiliza bila kutia neno zaidi ya kusema "Heeh" na kumfanya Nuro aendelee na maongezi.
“Sasa hivi karibuni ndio nimekuja kugundua kuwa 'boss' na Noor wana urafiki mkubwa, tena kuna biashara wanashirikiana..”
“Duuh.. Makubwa haya!” Rukia alijikuta akihamaki.
“Ndo hivyo mama, madogo yana nafuu..” Nuro aliongea kirafiki zaidi wakati huu, sio kama mtu anayeongea na boss wake.
“Sasa kama boss anashirikiana na Noor sisi tutakua na la maana kweli? Maana yule Noor ndiye ambaye muda wote anafikiria kumlinda Khatib tu” Rukia alionyesha kuchoshwa na maelezo haya.
“Ndo hivyo, Noor ndiye chanzo kikubwa cha Ahmed kumuua Alice, nadhani unakumbuka, yule baba ni hatari kuliko hata huyo Khatib mwenyewe”
“Nakumbuka, uliniambia, kwahiyo hata hizo damu za watu wasio na hatia kina Alice na Sauda tutaziacha ziteketee hivyo” Rukia alionyeshwa kukerwa sana na Ally Ngoswe..
“Ndo hivyo, fuata 'order' Detective, tusije na sisi tukapotea buree”
“Hilo nalo nenoo..” Alimalizia hvyo Rukia kisha wakaagana na kukata simu.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Kuwa mtu wa busara, toa sana sadaka, onyesha kila unachomiliki ili watu wakujue vizuri..kwakweli utaishi kwa amani sana” Mzee J4 aliamua kutoa ushauri wake. Khatib alikuwa bado yupo kimya akimsikiliza.
“Kwakweli ukiwa muwazi hakuna mtu atayekufikiria vibaya, kwani wangapi wamerithi mali za baba zao hapa nchini kwetu na bado wanaonekana watu wazuri tu kwenye jamii? Sasa wewe pia si inasemekana umerithi? Kwanini machoni pa watu usiwe mzuri? Acha mambo ya ajabu kuanzia sasa, jiweke juu kama mfano, watu watakuheshimu, hebu watoe wasiwasi watu ndugu yangu, watu wamekuwa na wasiwasi na wewe..waonyeshe kuwa wewe ni mtu mzuri, kwanini unaendelea kujizolea sifa mbovu wakati nafasi ya kusawazisha unayo?” Mzee J4 aliongea maneno toka moyoni.. Na alifanikiwa kuyapenyeza maneno yale moja kwa moja kwenye moyo wa Khatib. Ila katika kichwa cha Khatib kulikuwa na maswali mengi sanaa, kwanini huyu Mzee anamtaka afanye hivi? Yeye anafaidika nini? Na kwanini amshauri mambo hayo wakati anafahamu ukweli kabisa kuwa alimuua Sauda? Kwanini bado yuko upande wake na kumsihi abadilike? Au Mzee J4 alikuwa anahitaji kitu kutoka kwake? Maswali yote hayo hayakujibika katika kichwa chake.
“Mzee mimi nimekuelewa sana, na nakuahidi nitalifanyia kazi hilo ndani ya muda mfupi” Khatib alimuahidi Mzee J4, ila alikuwa na swali ambalo alipanga lazima amuulize leo.
“Ila natamani kujua hizi habari zote wewe unazijuaje, mpaka kufikia kunambia kwa kujiamini kuwa nimemuua mke wangu?”
“Mimi najua kila kitu unachofanya, na kila hatua unayopitia, najua kuwa wewe jina lako Mwatete Mwinjuma, najua pia kuwa ulitokea katika familia ya kimasikini tu na ukaja kusaidiwa kimaisha na mzungu mmoja mwenye asili ya Canada na baadae kumfanya mwanamke wako licha ya kuwa amekuzidi miaka 24, na najua pia kuwa unamiliki Euler Hotel na Mambo Pub pale Morogoro pamoja na ile Hotel ya Dar anayosimamia mamaako, nafahamu vizuri pia ushauri wako uliompa Hisham muda mfupi uliopita ukitaka amuue mkewe, na hata kabla hujakuja nyumbani leo nafahamu ulikuwa Hotel na mama wa mtoto wako Abdul ambaye umemwachia milioni 1.3 wakati mnaagana.. Kiufupi nakujua sana ndani nje, mimi naijua HISTORIA BATILI yako, na nina nafasi kubwa sana ya kukufanyia vyovyote utakaponikera..” Mzee J4 alifunguka kuhusu HISTORIA BATILI ya Khatib ambayo ilikua ikijulikana kuwa alikulia katika maisha ya kitajiri na kumbe si hivyo.. Hapa Khatib aliduwaa.
“Kunikera kwangu ni kutofuata ninachokushauri, nimekusamehe moja kwa moja kwa kumuua kipenzi cha mdogo wangu nimpendaye.. Lakini siku zijazo sitakusamehe kwa lolote, hivyo naomba twende sawa kutokea sasa”  Mzee J4 alionekana kubadilika ghafla, Khatib alikua kwenye wakati mgumu sana ambao hakuwahi kuutegemea.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Haya sasaa.. Fumbo la muda mrefu linafumbuliwa na Mzee J4, tunaanza kuijua HISTORIA BATILI ya Khatib. Hapa ndipo story yetu inapoanzia..
Utamu unaanza hapaa...

Ila kwa leo, tukomee hapa..
Tukutane Episode ya 023.

Usiache kufollow IG:@ jk.stories kwa story tam zaid, updates na mambo mengine kibaaaaoooo..
Kaa tayari pia kusoma kitabu cha HISTORIA BATILI kinakuja hivi karibuni.
Una maswali? Maoni? Usiache kuandika kupitia mdharuba@gmail.com
Au
Call/sms @ +255718274130/+255654727266